Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu nchini Sudan (SFA) ya kuomba Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano yao ya Sudan Super League yanayoshirikisha jumla ya timu Tatu.

SFA wameomba kucheza michezo hiyo hapa nchini katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ikiwa ni sehemu ya kurudisha Amani nchini kwao kufuatia kuwepo kwa machafuko ya kisiasa yaliyopelekea kushindwa kuandaa mashindano ya ligi nchini kwao.

Kwa upande wa SFA wanaamini kupitia shindano hilo la Sudan Super League itawasaidia wananchi wa Sudan kurudisha umoja wao na kufurahia kuona timu zao zikicheza tena baada ya kutofanya hivyo kwa muda sasa.

Michezo ya Super League inatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 25 -30 mwaka huu wa 2024 ambapo kila siku kutakua na mchezo mmoja huku timu shiriki zikiwa ni Al Hilal SC, Al Merrikh na Al Wadi Nyala zote za Sudan. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement