SHEREHE ZA UFUNGUZI WA MICHEZO YA OLIMPIKI MJINI PARIS ZITAKUWA ZA MUALIKO MAALUMU
Zikiwa zimesalia takribani siku 98 kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki ya Paris nchini Ufaransa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris zinaweza kuhama kutoka Mto Seine iwapo hali ya usalama haitakuwa sawa kama wanavyotarajia.
Sherehe za ufunguzi zinatazamiwa kuwa za kwanza kufanyika nje ya uwanja huku zaidi ya wanariadha 10,000 wanatarajiwa kusafiri kwa umbali wa kilomita 6 wa Seine kwa mashua 160.
Tayari imefichuka kuwa watalii hawatapewa fursa ya bure kutazama sherehe hiyo, kama ilivyopangwa awali. Badala yake, tikiti zitakuwa kwa mwaliko pekee, sio kupitia usajili wazi.
Lakini Rais Emmanuel Macron ameeleza kuwa Michezo ya Olimpiki itaendelea kuwa na manufaa kwa jamii na pia isiyochafua mazingira na isiyo na ubadhirifu,
Michezo Adilifu ya Majira ya joto huko Paris inaweza kusaidia kuishi kwa muda mrefu kwa hafla kuu ya IOC.
Mbali na kuendelea kwa maandalizi makubwa kwaajili ya michuano hiyo lakini imetaarifiwa kuwa Usalama bado ni changamoto kwa jiji hilo ambalo limekumbwa mara kwa mara na ghasia mbaya za itikadi kali.
Wasiwasi wa usalama umeongezeka kufuatia vitisho vya kundi la Islamic state (IS) kwa mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Paris, Madrid na London.
Mashindano ya Olimpiki yanatarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11 mwaka huu huku Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ikifuata kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu.