Shabiki wa Yanga ajulikanaye kwa jina la Alex Mayaya mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Katoro Mkoani Geita ameuawa na walinzi wa duka lake usiku wa saa tisa baada ya yeye kuingia katika duka lake akiwa amelewa na kutoa mataili mawili ya pikipiki huku walinzi wa duka hilo wakamvamia na kumpiga wakidhani ni mwizi kwani walinzi hao walikuwa awamfahamu vizuri kwani duka hilo linasimamiwa na Mtoto wake.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Geita ACP Safia Jongo amesema walinzi waliomuua wanatoka kampuni ya SAMIKE SECURITY huku akitoa Rai kwa walinzi wa makampuni kutojichukulia Sheria mkononi badala yake waarifu wawafukishe kituo Cha Polisi kwa hatua Zaidi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement