Shirikisho la Soka la Saudi Arabia SFF limeghadhabishwa na ishara ya mkono ya Ronaldo kwa mashabiki wa klabu ya Al Shabaab walioimba jina la Messi.

Nyota wa Ureno na Al-Nassr Cristiano Ronaldo, amejikuta kwenye utata baada ya Kamati ya Nidhamu ya Ligi Kuu ya Roshni nchini Saudia kudokeza kuwa 'itachukua hatua muhimu' dhidi yake.

Cristiano Ronaldo alitoa ishara kwa mashabiki uwanjani Saudi Arabia baada ya timu yake ya Al Nassr kuifunga Al Shabab 3-2.

Ronaldo, alikuwa akiwajibu mashabiki wa timu pinzani ambao "walimsumbua" kwa muda mrefu mechini na maneno ya "Messi, Messi," na kumlazimu mchezaji huyo kuwafanyia ishara isiyoruhusiwa.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Saudi Arabia, vinaripoti kuwa gwiji huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid ameadhibiwa kwa vitendo hivyo vyake na atakosa michezo miwili ijayo ya Al Nassr pamoja na kutozwa faini.

Cristiano Ronaldo ambaye alifunga mojawapo ya mabao ya timu yake, licha ya kuwa mfungaji bora katika ligi hiyo ya Saudia kwa mabao 22, matatu mbele ya mpinzani wake wa karibu, Mserbia Aleksandar Mitrovic, Ronaldo amekuwa akilengwa kwa nyimbo kama hizo katika mechi nyingi katika msimu wa sasa wa ligi ya Kiarabu.

Aidha, inadaiwa kuwa Ronaldo atakosa mechi ya ligi kati ya klabu yake Al Nassr na Al-Hazm siku ya Alhamisi na pia huenda akakosa kushriki ngarambe ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa bara Asia ya Al Nassr.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement