Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema kwa sasa serikali imejikita katika ujenzi wa Viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya mashindano sambamba na mashindano ya AFCON 2027.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma ambapo ameliambia Bunge kuwa mbali na ujenzi wa Uwanja wa Arusha, maeneo ya kupumzika Dodoma na Dar es Salaam , ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru Jijini Dar es Salaam lakini ameshatembelea Uwanja uliopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambao utatengenezwa ili uweze kutumika kwa ajili ya mazoezi ya timu zitakazokuwa jijini Arusha kipindi cha mashindano ya AFCON 2027.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement