Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ya Awamu ya Sita imepanga kujenga uwanja mpya wa Kimatafa wa Gofu katika eneo la Chamwino jijini Dodoma.

Dkt. Ndumbaro amesema hayo Jijini Arusha alipokua akifungua Mashindano ya Kimataifa ya Gofu.

“Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, DKT: Samia Suluhu Hassan imejipambanua katika kuendeleza michezo, tunafahamu namna ambavyo Rais ameendeleza michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa gofu, katika Gofu mahususi Mheshimiwa Rais ameshatamka wazi na kutoa maelekezo kwamba Serikali itajenga Uwanja wa Gofu katika Ikulu ya Chamwino pale Dodoma, ” Damas Ndumbaro – Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Amesema tayari Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo juu ya ujenzi wa uwanja huo ambao utachangia kuibua vipaji na kuendeleza Sekta ya michezo hapa nchini.

Mashindano hayo yatafanyika kwa siku nne ambapo wachezaji wa Kimataifa kutoka nchi mbalimbali wanashiriki ikwemo, Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Zambia ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kutoka kwa waandaaji zinashindaniwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement