Klabu ya SC Villa ya Uganda imetwaa Kombe la Ligi Kuu baada ya miaka 20 kupita.

SC Villa wameibuka Mabingwa baada ya kukusanya point 57 wakifuatiwa na Bul FC na Vipers wenye point 56 kila mmoja. 

Ligi ya Uganda imetamatika leo na sasa klabu hiyo itaiwakilisha Uganda katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Mara ya mwisho SC Villa kutwaa kombe la Ligi Kuu Uganda ilikuwa chini ya kocha Sam Timbe mwaka wa 2004.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement