Utata umegubika kwenye pambano la RS Berkane dhidi ya USM Algiers ambapo nusu fainali hiyo ya shirikisho Afrika imeshindwa kupigwa jijini Algiers nchini Algeria kutokana na kuwa Berkane wana jezi zenye ramani kamili ya nchi ya Morocco ikiwemo eneo la Western Sahara, hii ikiwa tofauti na siasa ya Algeria ambapo wao wapo upande wa uhuru wa Western Sahara kutoka kwa Morocco. 


Algeria wanawapa nguvu kundi maarufu la Polisario Front separatist movement, ambapo agenda yao ni Western Sahara iwe huru! Kutokana na hilo Berkane walizuiwa Airport kwa muda mrefu na waliswali swala ya Ijumaa hapo na walifanya mazoezi mepesi, baadae waliruhusiwa kuondoka ila jezi zilizuiwa kutoka ikitajwa Berkane wacheze mechi bila ramani ya Morocco kwenye jezi. 


Kutokana na sakata hilo shirikisho la soka la Morocco limetuma ndege binafsi kuwachukua Berkane na kurudi nyumbani kwakuwa mzigo wa jezi imeshindikana kuzitumia, mechi imeghairishwa rasmi tukisubiri maamuzi kutoka CAF.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement