Mchezaji wa Arsenal Bukayo Saka amejitolea kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Morocco kwa kujenga kijiji cha makontena yatakayotoa makazi kwa familia 84, pamoja na watoto 89.

Winga matata wa viongozi wa ligi kuu ya Uingereza, Arsenal na England mwenye umri wa miaka 22 alichangia makontena 50 kwa jamii katika eneo la Taroudant, ili kutoa makazi kwa watu 255.

Miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa sana na tetemeko la ardhi yalikuwa Al Haouz, Taroudant, Chichaoua, Marrakech, Ouarzazate, Youssoufia, Tinghir, Azilal, na Agadir.

Mchango huo kutoka Saka alioufanya kupitia Shirika la Misaada ya Matibabu kwa watoto BigShoe, umewanufaisha wakazi wa kijiji kilichowapoteza kati ya watu 3,000 waliofariki katika msiba huo.

"Shukrani Kwa Bukayo Saka, sasa watoto wanapokea msaada, wana paa juu ya vichwa vyao tena na tabasamu kwenye nyuso zao," BigShoe ilisema katika chapisho lake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement