Kinara wa soka wa Senegal, Sadio Mane alisema kuwa michuano ya Afcon 2023 haipaswi kuchezwa mapema majira ya saa nane mchana.

Kulingana na hali ya joto la juu lenye kuzidi nyuzi joto 30, mechi za kwanza kuchezwa saa nane jua kali si jambo ambalo linapaswa kufanyika katika karne hii.

Akishangazwa na hilo amesema pia ulimwengu unataza Afcon na iwapo wanataka kuona ubora wa wachezaji hawapaswi kuchezesha mchana.

Kocha wa Gambia amesema hana haja ya kutafuta visingizo kutokana na hali ya hewa kwani kila timu inapambana katika eneo moja na sawa.

Senegali waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gambia kwenye mechi yao ya kwanza hapo jana Jumatatu katika mji mkuu Yamoussoukro, Ivory Coast.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement