Kiungo mkabaji wa Simba, Sadio Kanoute ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Prisons utakaochezwa kesho Machi 6, 2024 kwenye Uwanja wa CCM Jamhuri, Morogoro kutokana na kuwa majeruhi.

Kanoute ataukosa mchezo huo baada ya kusumbuliwa na majeraha ya nyonga aliyoyapata kwenye mchezo wa Kombe la Azam (ASFC) dhidi ya TRA uliochezwa Februari 28, 2024 Azam Complex, Simba ilipopata ushindi wa mabao 6-0 huku kiungo huyo akifunga hat-trick.

Akizungumza na waandishi wa habari, kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema wachezaji wamejiandaa kupambana licha ya kumkosa kiungo huyo muhimu.

"Tunatarajia kumkosa Sadio Kanoute kwenye mchezo wa kesho na hilo linatokana na kwamba anaendelea kusumbuliwa na changamoto ya nyonga, kwakuwa tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kupewa maelekezo wakacheza tumejiandaa kisaikolojia."

“Kumkosa mchezaji kama Sadio kwenye timu yetu ni pigo kubwa kwakuwa amekuwa na umuhimu wa aina yake hususani pale anapoanzishwa kikosini lakini kwa sasa tunachofikiria ni kupata matokeo."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement