Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa taarifa ya kwa nini Nahodha wa timu ya Taifa, 'Taifa Stars', Mbwana Samatta hajaitwa kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mashindano ya FIFA Series 2024.

Taarifa hiyo imesema Samatta ameomba kutojumuishwa kwenye kikosi hicho ombi ambalo limekubaliwa.

"Nahodha wa Stars, Samatta ameomba kutojuishwa kwenye kikosi kilichoitwa kwa michezo ya FIFA Series na alizungumza na kocha kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kuomba ombi hilo ambalo limekubaliwa," imesema taarifa hiyo.

Kikosi cha wachezaji 23 kilichoitwa leo na Kaimu Kocha Mkuu, Hemed Suleiman 'Moroco' kwenye eneo la washambuliaji kimemwacha nahodha Samatta na kuwaita Clement Mzize (Yanga), Saimon Msuva (Al najmah FC, Saudia), Kibu Denis (Simba), Abdul Suleiman (Azam FC), Ben Starkie (Likeston Town, Uingereza) na Charles M'mombwa (Macarthur FC, Australia).

Makipa ni Aishi Manula (Simba), Aboutwaleeb Mshery (Yanga), Kwesi Kawawa (Syrianka FC, Sweden) huku mabeki Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad (Yanga), Mohamed Hussein na Kennedy Juma (Simba), Novatus Dismas (Shakhtar Donestsk, Ukraine), Miano Danillo (Villena) na Haji Mnoga wa Aldershot Town ya Uingereza.

Eneo la Viungo kuna Feisal Salum na Yahya Zayd wa Azam FC, Mudathir Yahya (Yanga), Morice Michael (RFK Novi Sad, Serbia), Himid Mao (Tala'ea El Gaish SC, Misri) na Tarryn Allarakhia anayekipiga Wealdstone, Uingereza.

Kikosi hicho kitaingia kambini machi 17, 2024 na kitaondoka Machi 18. Kitacheza michezo miwili na Bulgaria na Mongolia michezo machi 22 hadi 25.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement