Michuano ya mipya ya African Football League inakabiliwa na changamoto nyingine baada ya klabu ya TP Mazembe ya DRC kuripotiwa kugoma kuvaa jezi yenye Nembo ya 'Visit Rwanda' kwenye mashindano ya African Football League kutokana na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Itakumbukwa, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilitangaza kuingia ushirikiano na Serikali ya Rwanda, kupitia Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Wizara ya Michezo, na RwandAir ambao unalenga kuendeleza soka na utalii barani Afrika kupitia Ligi mpya ya Soka ya Afrika (AFL) itakayoshirikisha vilabu bora vya soka barani humo.

Aidha taarifa ya CAF ilibainisha kuwa AFL itafanya kazi na Wizara ya Michezo na Shirikisho la Soka ya Rwanda (FERWAFA) katika mipango ya maendeleo ya soka ya vijana, ikiwa ni pamoja na kuendeleza ligi ya ndani ya vijana.

Ndege ya taifa ya Rwanda, RwandAir itakuwa mshirika wa shirika la ndege la ligi hiyo na itasafirisha timu shiriki hadi nchi ambazo ni miongoni mwa njia zake.

Akizungumzia ushirikiano huo, VĂ©ron Mosengo-Omba, Katibu Mkuu wa CAF, alisema: "Ushirikiano na "Visit Rwanda" ni hatua kubwa. Nina furaha kutangaza ushirikiano wetu wa kusisimua na taifa ambalo linaonyesha ari ya ukuaji na uwezo wa soka la Afrika. Pamoja. tutafungua upeo mpya wa mchezo mzuri kwenye Bara Letu, tukionyesha shauku ya mashabiki wetu. Hatuwezi kusubiri kuanza safari hii ya ajabu pamoja na "Tembelea Rwanda".

Hatua ya TP Mazembe kuchomoa ni kizungumkuti kingine kuelekea ufunguzi wa michuano hiyo siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement