Wiki hii ilikuwa ya moto sana kule Ulaya ambapo kulikuwa na michezo minne ya hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Jumanne na Jumatano.

Ukiondoa tishio la shambulio la kigaidi lililotolewa na kundi ISIS, moja kati ya vitu vilivyonogesha michuano hiyo ilikuwa ni saa ya USD 1, 500, 000 sawa na Sh3.5 bilioni aliyoivaa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alipokuwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati timu yake inavaana na Real Madrid, Jumanne.



Saa hiyo aina ya Calibre RM27-01, imetengenezwa na kampuni ya Richard Mille na awali ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya mchezaji wa tennis Rafael Nadal na dunia nzima hadi kufikia sasa zipo 50.

Saa hiyo inashikilia rekodi ya kuwa saa nyepesi zaidi ya mkononi kuwahi kutengenezwa ikiwa na uzito wa gramu 18.83.



Katika mchezo huo Man City ilifanikiwa kupata sare ya mabao 3-3 ambayo yalifungwa na Bernardo Silva, Phil Foden na Jasko Gvardiol huku ya Madrid yakifungwa na Rodrygo, Federico Valverde na moja lilikuwa la kujifunga kwa Ruben Diaz.

Sare hiyo inaonekana kuwa nzuri kwa Manchester City ambayo itakuwa nyumbani katika mechi ya marudiano itakayochezwa kwenye uwanja wa Etihad Jumatano ya April 17, 2024.






You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement