ROY KEANE: TEN HAG ANATAKIWA KUTHIBITISHA MANCHESTER UNITED INAELEKEA SEHEMU SAHIHI
Phil Foden alifunga mabao mawili katika kipindi cha pili, Manchester City na kuambulia ushindi muhimu wa 3-1 dhidi ya wapinzani wao Manchester United, Kufuatia kipigo cha 11 cha Premier League msimu huu, Roy Keane anasema Erik ten Hag bado anatakiwa kuthibitisha kuwa timu yake inaelekea kwenye mwelekeo sahihi.
Mabingwa hao walishangazwa na bao zuri la Marcus Rashford baada ya dakika nane pekee lakini ndio waliotawala katika pambano kali la Ligi ya Premia.
Man city juhudi zao zilizaa matunda kwani Phil Foden alisawazisha kwa juhudi za masafa marefu katika dakika ya 56 na kuweka timu yake mbele zikiwa zimesalia dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika. Erling Haaland aliweka matokeo mapya ubaoni na mchezo huo kumalizika 3-1.
Ushindi umeifanya City kuwa nyuma kwa pointi moja dhidi ya vinara Liverpool kabla ya timu hizo mbili kukutana katika uwanja wa Anfield wikendi ijayo. Lakini nini kitafuata kwa United kufuatia kipigo cha 11 cha Premier League msimu huu.
"Siwezi kuwa mgumu sana kwa Manchester United leo kwani City walikuwa na kipaji," Keane alisema. "Walionyesha kwa nini wao ni mabingwa. Hiyo ni hasara ya 11 kwenye ligi kwa United. Hiyo ni takwimu ya kutisha na wanachofanya City ni kugundua mapungufu yako yote.