Mechi za Mkondo wa pili Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League kutimua vumbi hii leo kwa michezo miwili, Borussia Dortmund wakiwakaribisha Atletico Madrid huku PSG akiwa ugenini dhidi ya Barcelona.

Kocha wa Borussia Dortmund Edin Terzic ameweka wazi kuwa timu yake italazimika kutoa kila kitu katika mechi yahii leo baada ya kupoteza mbele ya wapinzani wao kwa bao 2-1 katika mchezo wa kwanza.


Katika mchezo huo, Dortmund itamkosa mfungaji wa bao moja la mchezo wa mkondo wa kwanza Mshambuliaji Sébastien Haller ambaye ameondolewa kwenye mechi kutokana na jeraha lake la kifundo cha mguu wa kushoto.

Kocha Terzic alithibitisha kuwa Haller aliumia kifundo cha mguu tena kwa bahati mbaya katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Borussia Mönchengladbach siku Jumamosi na sasa atakuwa nje ya Uwanja ka muda wa wiki moja huku akiongeza kuwa kutakuwa na uchunguzi zaidi siku ya jumamosi kuhusu majeraha yake ili kuamua wakati wa kupumzika kwa usahihi zaidi na wanafikiri unafikiri hatakuwepo kwa wiki mbili hadi tatu.

Mbali na mchezo huo lakini mchezo unaotazamwa kwa ukubwa zaidi ni PSG dhidi ya Barcelona ambapo Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez ameeleza kuwa wako tayari kwa vita dhidi ya PSG na kuongeza wachezaji wake wako tayari kuteseka ili kusonga mbele.


Xavi amesema kuwa timu yake sio ya kubahatisha wanajivunia walipo kwa sasa kwani lengo kubwa ni kushinda mchezo kwa kuonyesha ubora na haiba ya timu.

Kwa upande wake Kocha wa PSG Luis Enrique amesema licha ya kupoteza kwa bao 3-2 katika mchezo wa awali lakini anaimani ya kufuzu hatua inayofuata.

Mhispania huyo, ambaye aliiongoza Barca kushinda mataji matatu mwaka wa 2015 ameweka Imani kuwa PSG wangeweza kushinda kile alichofikiri ni kupoteza isivyo haki na kuendeleza harakati zao za kuwania taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa.

Enrique ameongeza kuwa Siku baada ya mchezo wa awai Robo Fainali ya Michuano hiyo zilikuwa ngumu kwao, lakini jambo zuri kuhusu soka ni kwamba kuna mchezo mwingine dhidi ya mpinzani huyo huyo na sasa wana wazo la nini wanapaswa kufanya na kuweka wazi kuwa Mechi ya kwanza ilikuwa na vita kali na timu zote mbili lakini matokeo hayakuonyesha kile walichostahili, matokeo ya bao 3-2 yaliwaonyesha kuwa ni lazima waendelee kupambana.


Beki wa pembeni wa PSG Achraf Hakimi ambaye alikosa mechi ya kwanza kutokana na kusimamishwa hii leo anatazamia kuonekana Dimbani.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement