Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu inayoshiriki ligi kuu ya Uholanzi Heerenveen.

Mfungaji bora wa Uholanzi kwa upande wa wanaume, 40, amesaini mkataba wa miaka miwili na ataanza jukumu lake la kwanza la ukocha katika msimu wa joto.

Tangu alipostaafu kama mchezaji mwaka wa 2019, amefanya kazi kama kocha msaidizi katika klabu ya Feyenoord na amekuwa akisimamia timu za vijana chini ya umri wa miaka 18 na 19.

"Ningependa kuendeleza maendeleo yangu na jukumu la kocha mkuu linalingana kikamilifu na lengo hilo," alisema Van Persie, ambaye alikuwa sehemu ya timu ya United iliyoshinda Ligi kuu ya England mnamo 2013.

"Heerenveen ni klabu nzuri sana ya Primia Ligi yenye utamaduni mzuri na mashabiki waaminifu.

"Ni changamoto kubwa kuchangia katika malengo ya michezo na maendeleo ya klabu kama kocha mkuu."

Bosi wa sasa wa Heerenveen Kees van Wonderen alitangaza mnamo Machi kuacha jukumu hilo mwishoni mwa kandarasi yake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement