Kocha wa Klabu ya Simba, Roberto Oliviera "Robertinho" ameweka wazi kuwa, licha ya sare ya bao 2-2 dhidi ya Al Ahly kunako ufunguzi wa Michuano ya African Super League "AFL", katika Dimba la Mkapa, bado anaamini anauwezo wa kufanya vizuri na kusonga mbele kunako Michuano hiyo.

Kocha Robertinho ameeleza kuwa, anaimani na kikosi chake ambacho kimeonyesha kiwango Bora, huku akimpongeza mchezaji Mmoja Mmoja ndani ya Klabu yake.

Kocha Robertinho ameeleza kuwa, anaamini katika mchezo unaofuata ananafasi ya kufanya vizuri licha ya kuwa wapinzani wao ni timu Bora lakini kwakuwa malengo yake kwa Kila mchezo ni wakutafuta ushindi hivyo anaamini atafanya vizuri katika mchezo huo utakaopigwa Octoba 24 nchini Misri.

"Kila timu inapocheza inahitaji ushindi na Mimi malengo yangu kwa Kila mechi ni kupata ushindi, japo wapinzani wetu ni timu imara, ni Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, lakini mipango yangu ni kushinda, mpira unahitaji kuonyesha uwezo ulionao uwanjani nipo hapa kucheza vizuri na kushinda, "

Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo, Michuano hiyo ya AFL inaendelea hapo kesho kwa mchezo wa Petro De Luanda dhidi ya Mamelod Sundown utakaopigwa kunako dimba la Estadio 11 de Novembro nchini Angola.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement