RICARDO FERREIRA KUINOA SINGIDA FOUNTAIN GATE ILI KUPATA USHINDI
Mkataba wake ni wa mwaka mmoja kuwanoa mastaa wa Singida Fountain Gate, inayoshiriki Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere, Beno Kakolanya, Bruno Gomes, Pascal Wawa,
Kocha Ricardo Yupo na msaidizi wake ambaye ni Andrew Barbosa hawa watafanya kazi kwa kushirikiana ndani ya timu hiyo.
Ricardo Ferreira amechukua mikoba ya Ernest Middendrop aliyekuwa kocha wa timu hiyo na kuachia ngazi baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho Afrika.