Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Nchini Zambia Red Arrows FC wamekata tiketi ya mwisho ya kutinga hatua ya nusu fainali michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024 mara baada ya kuitandika ASAS Djibouti Telecom bao 1-0 katika mchezo wa Kundi B uliochezwa dimba la KMC jijini Dar es salaam.

Red Arrows ilihitaji kpata ushindi ili kuweza kumaliza na pointi sita na kufuzu kama timu iliyo nafasi ya pili mbele ya SC Villa ya Uganda iliyomaliza na pointi 5.

Katika mechi nyingine iliyochezwa Al Hilal waliwashinda Gor Mahia 2-0 na kuweka rekodi yao ya ushindi katika mashindano ya hayo. 

Florent Ibenge, Kocha wa Al Hilal alisema licha ya wachezaji wake kuumia, anafurahi wameshinda mechi zote tatu na kutinga nusu fainali. 

APR ya Rwanda sasa itamenyana na Al Hilal katika hatua ya nusu fainali, huku Hay Al Wadi FC ikimenyana na Red Arrows.

Mechi zote za nusu fainali zitapigwa siku ya Ijumaa huku fainali ikichezwa siku ya Jumapili.

Bingwa wa Michuano hii atajinyakulia kitita cha Dola za Marekani 30,000 huku timu itakayoshika nafasi ya pili ikiondoka na Dola 20,000 na wa tatu Dola 10,000. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement