Fainali yenye kuvutia wengi hii leo kwa maana ya Jumamosi ya Juni 01, Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Maarufu kama UEFA Champions League kwenye Uwanja wa Wembley ni Borussia Dortmund ambao watakutana na Real Madrid katika Fainali hiyo.

Dortmund imekuwa timu ya kushangaza kwa maana ya “SURPRISE PACKAGE” katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu huu machoni wa watu wengu ikipitia kundi gumu zaidi kabla ya kuwatoa PSV, Atlético de Madrid na Paris Saint-Germain hatimaye kufanikiwa kutinga fainali.

Walianza hatua ya Makundi wakiwa Kundi F na PSG, Milan na New Castle.

Pia washindi wa kundi C kwa maana ya Real Madrid walimaliza hatua ya Makundi wakiwa na pointi 18 akiwa na Napoli, Braga na Union Berlin.


Madrid walipitia majaribio makali katika mechi zao zote za mtoano na kutinga fainali, wakielekea ukingoni dhidi ya Leipzig, Manchester City na Bayern kabla ya kutinga fainali yao ya 18 katika shindano hili. 

Real waliwashinda mabingwa Manchester City kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya nane bora na kufunga mabao mawili ya dakika za lala salama katika mkondo wa pili wa nusu fainali na kuwashinda Bayern Munich.

Madrid hawajafungwa katika mechi zao 12 za shindano msimu huu, wakishinda mechi nane na kutoka sare Mechi nne kwamaana ya (W8 D4) na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwao kufika fainali ya Kombe la Ulaya/Ligi ya Mabingwa bila kupoteza mechi. 

Dortmund wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 11 ya mwisho za Ligi hiyo wakishinda Michezo saba na wakitoka sare michezo mitattu kwamaana ya (W7 D3), ingawa walisawazisha bao katika mechi sita kati ya hizo na kufunga bao la kwanza katika mechi tisa kati ya kumi zilizopita.


Fainali ya mwisho ya Borussia Dortmund ya Ligi ya Mabingwa pia ilifanyika kwenye Uwanja wa Wembley, ambapo walifungwa 2-1 na Bayern mwaka 2013. 

Uzoefu huo utakuwa muhimu dhidi ya timu ya Madrid ambayo si ngeni kwenye mchezo mkubwa zaidi katika soka la Klabu za Ulaya na ambayo imepoteza mechi moja tu kati ya 20 za mwisho za UEFA dhidi ya timu za Ujerumani (W13 D6).

Real Madrid wanyerekodi ya kubeba kombe hili mara 14 watavaana na Dortmund waliobeba Kombe hili mara moja pekee.

Matumaini makubwa ni kwa Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti akiwa kocha aliyefanikiwa zaidi kwa kubeba mataji manne katika shindano hili tofauti na Dortmund ambao hawakuwa na msimu mzuri katika Ligi lakini wakaonekana kufanya vizuri barani Ulaya.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement