Kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois atakuwa nje kwa miezi miwili baada ya kupata majeraha akiwa mazoezini leo mchana.

Courtois mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akifanya mazoezi ya kurejea tena katika hali ya utimamu wa mwili baada ya kuwa nje akiuguza majeraha ya goti aliyoyapata mapema mwanzoni mwa msimu huu.

Inalezwa kuwa vipimo vya awali vimeonyesha 'meniscus' yake katika goti la kulia imejeruhiwa na atalazimika kufanyiwa upasuaji tena ili awe sawa.

Upasuaji huo mpya unakadiriwa kuwa utamuweka tena nje kwa miezi miwili hadi mitatu hali inayoweza kumsababishia kukosa michuano ya Euro inayotarajiwa kuanza Juni 14, mwaka huu.

Ili kuziba nafasi yake baada ya kuumia, mabosi wa Real Madri walimsajili Kepa Arrizabalaga kwa mkopo kutoka Chelsea. Mbali ya Kepa, pia Madrid imekuwa ikimtumia kipa wao raia wa Ukraine Andriy Lunin.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement