Klabu ya Real Madrid imetengua kauli na kuthibitisha kuwa itashiriki michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu vya FIFA, mashindano ambayo vilabu mbalimbali kutoka Afrika kama Mamelodi Sundowns vitashiriki.

"Hakuna shaka, tutakuwa sehemu ya Kombe la Dunia na tunajivunia kushindana ili tuweze kushinda kombe kwa ajili ya mashabiki wetu".

Saa chache zilizopita Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti kupitia mahojiano yake na Il Giornale alisema wamepanga kugomea michuano hiyo wakidai mapato yatakuwa ni madogo kwa klabu kubwa kama hiyo.

"Real Madrid haitashiriki Kombe la Dunia la vilabu, tutakataa mwaliko wao".

"Mechi moja ya Real Madrid ina thamani ya €20m (sawa na Tshs Bilioni 56) wao ​​wanataka kutupa pesa hizo kwa shindano zima… hapana”,

Tutaishuhudia Real Madrid kombe la dunia la Vilabu mwaka 2025.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement