Rais wa Klabu ya Yanga SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Mhandisi Hersi Said ameitembelea klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa na kukutana na baadhi ya mastaa wa timu hiyo pamoja na Rais wa kikosi hicho.

Hersi amekutana Rais huyo na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris nchini Ufaransa, jana.

Mhandisi Hersi alipewa mualiko maalum kutoka kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.

Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0.

Licha ya Hersi kuonana na rais huyo, lakini pia amekutana na wachezaji Kylian Mbape, Marquinho na Achraf Hakimi na kupiga nao picha za ukumbusho.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement