RAIS WA VYAMA VYA SOKA AFRIKA MASHARIKI NA KATI WALLACE KARIA AMEZIPONGEZA TIMU SHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA CACAFA DAR PORT KAGAME CUP 2024
Rais wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati "CECAFA" Wallace Karia ameweka wazi kuwa licha ya kukosekana kwa baadhi ya timu zilizotarajiwa kuleta ushindani zaidi katika mashindano ya CACAFA Dar Port Kagame Cup 2024 lakini mashindano hayo yameweza kuwa bora kwa timu ambazo zimeweza kushiriki.
Rais Karia ameeleza hayo mara baada ya kutamatika kwa Fainali ya michuano hiyo kwa Red Arrows ya Nchini Zambia kuibuka Mabingwa dhidi ya APR ya Rwanda walioingia nao katika hatua ya Fainali.
Kwa upande mwingine Rais Karia ameongeza kwa kuwapongeza Manispaa ya Kinondoni kuwa na Uwanja wenye ubora ambao umefanikisha mashindano hayo kuwa bora huku akiweka waiz juu ya matumizi ya Uwanja huo kwa msimu ujao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.