RAIS WA SHIRIKISHO WA MPIRA WA MIGUU CAMEROON (FECAFOOT) AMEKUJA NA SHERIA YA SUTI
Rais wa facafoot nchini Cameroon bwana Samuel Et'oo Ameamua Msimu ujao katika ligi kuu ya Cameroon pamoja na ligi daraja la kwanza ya kwamba vazi la SUTI ndio litakua maalum kwajili ya makocha na itakua ni lazima.
Sasa kocha mkuu ni lazima avae SUTI iwe LIGI KUU au ligi daraja la kwanza sasa uamuzi huo unakuja kwakua alie amua ni Rais wa shirikisho la mpira nchini Cameroon FECAFOOT kwa lengo la kuwaongezea thamani makocha lakini pia kua na muonekano ulio bora ili kufanya ligi ya Cameroon kua ya TOFAUTI kwani Et'oo anaamini makocha wakivaa hivyo itawaongezea thamani sana lakini SUTI ni vazi la heshima.
Katika Sheria hii mpya kama utakiuka basi adhabu yake ni dollar 111563.80 sawa na Zaidi million 250 za kitanzania ndio itakua adhabu endapo kocha asipo vaa SUTI.
Lakini kwa upande wa makocha wasaidizi wao watavaa jezi za TIMU kama kawaida lakini endapo nao wakijiskia kuvaa suti sio jambo baya itakua ni herii.
Et'oo amekuja na uthubutu huu kwa manufaa ya mpira wa Cameroon japo wapo wanao pinga wakiamini si sawa kulingana na kile ambacho kinaendelea kwa Rais huyu zile shutuma zinazo mkabiri.