RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF AMEZIPONGEZA TIMU ZINAZOSHIRIKI CECAFA DAR PORT KAGAME CUP
Rais wa Shirikisho la Soka chini “TFF” Wallace Karia amepongeza timu shiriki kunako mashindano ya CECAFA DAR PORT KAGAME CUP yaliyoanza kutimua vumbi hapo jana kwa maana ya Julai 09 katika Dimba la KMC sambamba na Chamazi Complex jijini Dar es salaam.
Rais Karia ameeleza kuwa amshindano haya yataweza kuzijenga zaidi timu zitakazowakilisha mataifa yao kunako mashindano ya Ligi ya mabingwa sambamba na Shirikisho Afrika.
Kwa upande wake Kocha wa Coastal Union David Ouma ambaye timu yake imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dekedaha ya nchini Somalia amekipongeza kikosi chake kwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo huo wa ufunguzi.
Matokeo mengine kunako michuano hiyo ni Al Wadi Nyala FC ambao wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU, SC Villa wakitoka sare ya bila kufungana dhidi ya El Merriekh na APR FC wakiitandika Singida Black Stars bao 1-0.
Michuano hiyo inaendelea kutimua vumbi hii leo kwa michezo miwili kupigwa kunako Dimba la Chamazi Complex, Al Hilal FC dhidi ya Djibout Telecom na Gor Mahia FC dhidi ya Red Arrows