RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA CAMERON SAMUEL ETO'O YUPO HATARINI KUKUMBANA NA ADHABU YA KUFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SOKA
Samuel Eto’o, Rais wa Shirikisho la soka la Cameroon yupo katika hatari ya kufungiwa kujihusisha na soka baada ya kuhojiwa Jumanne Juni 25 mjini Cairo, Misri na Mahakama ya nidhamu ya Shirikisho la soka la Afrika.
Mshambulizi huyo wa zamani wa FC Barcelona anakumbana na shutuma nzito za kupanga matokeo katika michuano ya Cameroon iliyoletwa dhidi yake na wachezaji wa soka wa Cameroon.
Samuel Eto’o anatuhumiwa pia kusaini makataba wa udhamini na Kampuni ya kubashiri kitu ambacho ni kiyume na taratibu mkataba kusainiwa na Rais wa shirikisho.
Uamuzi utaweza kutolewa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF siku zijazo nchini Misri ingawa ana hatari ya kufungiwa.