Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi amemsifu Kocha wa Klabu hiyo Luis Enrique kama meneja bora zaidi duniani baada ya kufanya kazi nzuri katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA.

Nasser Al-Khelaifi ameweka wazi kuwa Luis Enrique anastahili kuwa Meneja Bora zaidi Duniani baada ya kuwaondoa Barcelona na kufuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Kwa upande wa Dortmund ambao wamefanikiwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwatandika Atletico Madrid bao 4-2 hapo jana na kupelekea Agregate kusoma bao 5-4, Kocha Edin Terzic ameeleza kuwa ni jambo kubwa kwa klabu yetu na anajivunia timu yake.


Edin Terzic ameeleza kuwa Kulikuwa na nyakati mbili tena ambazo ziliwaumiza na zingeweza kuleta usawa, lakini hawakupoteza imani yeo kwa kile walichokitarajia. 

Robo Fainali ya Pili ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya utaendelelea kutimua vumbi hii leo kwa Bayern dhidi ya Arsenal huku Manchester City wakiwakaribisha Real Madrid.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement