Rais wa FIFA, Gianni Infantino atapamba mechi ya Kundi B ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kati ya Sudan Kusini na Sudan mnamo Juni 11, 2024.

Victor Lual, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Sudan Kusini (SSFA) aliithibitishia kwamba Infantino atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Uwanja wa Taifa wa Juba uliokarabatiwa ambao utakuwa mwenyeji wa mechi hiyo.

Lakini kabla ya pambano hilo la Juba, timu ya Sudan Kusini itasafiri kumenyana na Togo, huku Sudan nayo ikicheza ugenini dhidi ya Mauritania.

Kwa sasa Senegal wanaongoza Kundi B wakiwa na pointi 4 baada ya mechi mbili, huku Sudan walio nafasi ya pili wakiwa na pointi 4, lakini tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Sudan Kusini ambao wameambulia sare katika mechi mbili pekee ndio ambao wapo mkiani mwa kundi.

Timu nyingine katika Kanda ya CECAFA zinazomenyana katika mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 ni pamoja na; Djibouti, Ethiopia, Rwanda, Kenya, Burundi, Somalia na Uganda.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement