Kuelekea katika Mashindano ya Olimpiki 2024 Paris yatakayoanza Julai 26, makamu mkuu wa Rais wa Barbie na mkuu wa wanasesere duniani Krista Berger ameweka wazi juu ya kuchapishwa wanasesere wapya tisa wa Barbie wanaoonyesha baadhi ya wanamichezo wa kike mashuhuri zaidi duniani, akiwemo nyota wa tenisi Venus Williams na mwanasoka nyota wa Kanada Christine Sinclair. 

Krista ameeleza kuwa Wanasesere hao ni sehemu ya sherehe inayoendelea ya chapa hiyo ya maadhimisho ya miaka 65 ya Barbie huku wakitambua faida za michezo katika kukuza kujiamini, matamanio na uwezeshaji miongoni mwa kizazi kijacho huku akiongeza kuwa kwa kuangazia wanamichezo hao wenye msukumo na hadithi zao, wanatumai kutetea imani kwamba kila msichana anastahili fursa ya kufuata matamanio yake na kugeuza ndoto zake kuwa ukweli.

Wanamichezo wengine wanaotunukiwa na wanasesere wa Barbie katika mfanano wao ni Mwanamichezo wa Gymnastic au michezo ya kunyumbulika wa Brazil Rebeca Andrade , Alexa Moreno wa Mexico, mchezaji wa soka wa Australia Mary Fowler, bondia Mfaransa Estelle Mossely, muogeleaji wa Kiitaliano Federica Pellegrini, mwanariadha wa Kihispania Susana Rodriguez na mwanariadha kutoka Poland Ewa Swoboda. 

Mashindano ya Olimpiki 2024 yataanza Julai 26 mpaka Agost 11 mwaka huu kwa Matukio 329 katika michezo 32 kwa kushirikisha wanamichezo mbalimbali Duniani waliofuzu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement