Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe: Samia Suluhu Hassan amezipongeza Klabu za Simba na Yanga kwa kufanikisha matamasha yao na kuwataka kuangalia zaidi yaliyo mbele yao.

Akizungumza na mashabiki sambamba na viongozi wa Klabu ya Simba katika Tamasha la Simba Day, Rais Samia ameweka wazi furaha yake baada ya kuona mafanikio makubwa zaidi kwa msimu huu.


Kwa upande mwingine Rais Samia amewapongeza Yanga SC kwa usajili walioufanya kuelekea msimu mpya wa mshindano.

TUKIENDELEA KUSALIA KUNAKO TAMASHA LA SIMBA NA YANGA SC

Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ameeleza wazi juu ya maono yake kwa Klabu hizi mbili kufanya makubwa Kimataifa na kuweka wazi juu ya Derby baina ya timu hizi mbili kuwa Bidhaa ya Utalii Tanzania.

Naye mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba ambae ndiye Mwanzilishi wa Simba Day akiwa ni mjumbe wa Baraza la ushauri la Klabu hiyo kwa sasa Hassan Dalali ameweka wazi kufurahisha na muendelezo mzuri wa Tamasha hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitango cha Habari Yanga SC Ally Kamwe amefurahishwa na muitikio wa Mashabiki ambao waliweza kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na Uwanja wa Uhuru na kuweka wazi kuwa hiyo ni ishara njema kwao huku Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally akiweka wazi mafanikio kwa upande wao sambamba na suala la wachezaji ambao hawakuonekana kwenye utambulisho.

Dickson Job, Mchezaji wa Yanga SC ameelza juu ya wao kama wachezaji kuwa na deni kwa mashabiki waliojitokeza katika Tamasha lao la Kilele cha Wiki ya Mwanachi.


Kwa upande wa Mashabiki wa Simba SC ambao wametamatisha Tamashasha la msimu wa 16 la Simba Day sambamba na Wanayanga wakiwa wametamatisha tamasha la Msimu wa sita la Yanga Day wamezungumza.

Mbali na matukio ya Klabu za Simba na Yanga, lakini Azam FC wao kule nchini Rwanda waliweza kutambulisha wachezaji wao na benchi l ufundi katika Tamasha la Klabu ya Rayon Sports na Azam FC kufanikiwa pia kuondoka na Kombe la Rayon Sports Day.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement