RAIS SAMIA ATOA AHADI YA MILIONI 10 KWA KILA GOLI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi ya Tsh. 10 milioni kwa kila goli ambalo tutafunga katika mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly ambao utachezwa siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2023 saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Mkapa.