RAIS MWINYI AWAZAWADIA YANGA SC SHILINGI MILIONI 100 ZA PONGEZI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Klabu ya Yanga SC shilingi milioni 100, kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa waliopata katika msimu wa mwaka 2024/2025.
Rais Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 30 Juni 2025 alipokutana na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga waliofika Ikulu kwa ajili ya kumkabidhi makombe matano ya michuano mbalimbali waliyoyatwaa msimu huu.



