Professor Nabi Kuelekea Kaizer Chiefs
Nabi inasemekana tayari yupo mbioni kuondoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo huku akitarajia kulipwa takribani kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia ambapo ameweka sharti la kuja na wasaidizi wake akiwemo kocha wa viungo na mtaalamu wa kuwasoma wapinzani.
Mapema hivi leo kocha huyo amekutana na viongozi wa Yanga sc kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya ambapo inasemekana wameshindwa kukubaliana haswa katika masuala ya kimaslahi ikizingatiwa kuwa kocha huyo ana ofa hiyo nono kutoka Kaizer.
Wakala wa kocha huyo ambaye ni mwanae Hedi Nabi amesema kuwa bado haijajulikana kama ataondoka ama la mpaka amalize mazungumzo na Yanga sc kwanza ndio atajua kipi kinafuata.
“Siwezi kusema anaondoka wala anabaki kwasasa,b baba yangu ni mtu anayeheshimu viongozi mashabiki na hata wachezaji wake lakini kitu ambacho kitakwenda kutoa picha halisi ya baadaye ni pale atakapokutana na uongozi wa klabu yake,” alisema Hedi.