Baada ya jana mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube kufuta utambulisho na picha zote alizopiga akiwa na jezi za timu hiyo, leo ameendeleza kuonyesha kuwa haitaki tena timu hiyo licha ya kuwa ana mkataba wa miaka miwili na nusu kama klabu hivyo inavyodai.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Dube ameposti barua yenye ujumbe wa kuishukuru klabu hiyo akisema:

“Nikiwa katika hisia mchanganyiko natangaza kuondoka katika klabu ya Azam. Safari ya miaka minne kwangu ilikuwa njema sana iliyojaa ushindi, changamoto, furaha.”

“Nawashukuru wote kwenye klabu hii kuanzia uongozi, benchi la ufundi, wachezaji wenzangu na kwa upekee zaidi mashabiki wa klabu hii.”

“Ninavyoondoka kwenda kufungua ukurasa mwingine wa maisha yangu ya soka, naondoka na mafunzo yote mema niliyoyapata hapa na siku zote nitatangaza mazuri yote tuliyoyapata pamoja.”

“Naimani na uwezo mkubwa wa timu hii, naamini itaendelea kufanya vizuri na kufikia malengo, nawatakia kila la kheri na asanteni.”

Dube aliandika barua kuondoka Azam na kupewa masharti ya kufuata utaratibu wa kuvunja mkataba, licha ya kuwa hakuweza kuyafuata.

Ili kuvunja mkataba Dube, anatakiwa kuilipa Azam dola 300,000 ikiwa ni zaidi ya Sh750 milioni ambapo taarifa zinadai kuwa nyota huyo alipeleka nusu ya pesa na Azam walizikataa kwani anatakiwa kulipa zote kwa wakati mmoja.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement