Mpira wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2023 utakaofanyika nchini Ivory Coast kuanzia 13 Januari, umezinduliwa na CAF.

Imepewa jina la “Pokou” kwa heshima ya Laurent Pokou, gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast

Mpira huu una mchanganyiko wa rangi nyeupe, kijani na chungwa, rangi ya taifa la Ivory Coast.

Pokou alikuwa nani?

Pokou alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast, ambaye alikuwa mfungaji bora mara mbili wa AFCON, akifunga mabao sita katika mashindano ya 1968 nchini Ethiopia na manane katika dimba la 1970 nchini Sudan, yakiwemo matano katika mechi moja dhidi ya Ethiopia. ambayo Ivory Coast ilishinda 6-1.

Akiwa na jumla ya mabao 14, pia anakuwa mfungaji bora wa pili kwa jumla wa mashindano hayo, nyuma ya Samuel Eto’o wa Cameroon, ambaye alivunja rekodi ya Pokou katika AFCON ya 2008.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement