Saa kadhaa baada ya kutoka kwa taarifa za Paul Pogba kufungiwa kutojihusisha na soka kwa miaka minne kutokana na kuthibitika kutumia dawa za kutunisha misuli, Staa huyu wa Juventus amejibu kwa kusema maamuzi hayo sio sahihi na yamemshtua na kumuhuzunisha.

“Leo nimefahamishwa kuhusu uamuzi huo, ninaamini kuwa uamuzi huo sio sahihi, nimehuzunishwa, nimepata mshtuko na kuumia moyo kwamba kila ambacho nimejenga kwenye maisha yangu ya soka kimechukuliwa kutoka kwangu”

“Pale nitakapokuwa huru na vizuizi vya kisheria habari kamili itawekwa wazi lakini sijawahi kuchukua kwa kujua au kwa makusudi virutubisho vyovyote vinavyokiuka kanuni za kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli, kama Mwanamichezo wa kulipwa nisingeweza kamwe kufanya chochote kuboresha kiwango changu kwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku na sijawahi kuwadharau au kuwalaghai Wanamichezo wenzangu na Wafuasi wa Timu zozote nilizochezea au nilizocheza dhidi yao”

Pogba amemaliza kwa kusema kutokana na uamuzi uliotangazwa atakata rufaa kwenye Mahakama ya usuluishi wa michezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement