Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba ameripotiwa kufungiwa miaka minne kutojihusisha na soka baada ya kufeli majaribio ya dawa za kuongeza nguvu Agosti mwaka jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alipimwa na kukutwa na “testosterone” dawa za kusisimua misuli baada ya mechi ya kwanza ya Juventus msimu huu dhidi ya Udinese, na alipewa adhabu yake kali na ofisi ya mwendesha mashitaka wa kupambana na dawa za kusisimua misuli nchini Italia.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement