Pochettino amekiri kwamba Chelsea imefanya makosa makubwa kwa kutumia Pauni 1 bilioni kusajili mastaa wapya.

The Blues imeanza msimu vibaya huko kwenye Ligi Kuu England, wakishika nafasi ya 11 baada ya kushinda mechi tatu tu kati ya 10 walizocheza.

Chelsea mpya ya bilionea Todd Boehly ilianza vyema kwenye mechi za pre season, ambapo haikupoteza mchezo ilipocheza na Brighton, Newcastle na Fulham na kuamsha matumaini makubwa.

Lakini, baada ya ligi kuanza tu, mambo yametibuka huko Chelsea na timu imekuwa ikipata matokeo ya hovyo.


Kocha Pochettino anaamini hilo limetokana na namba ya wachezaji walioletwa na waliondoka kwenye dirisha la usajili, Kwenye dirisha la usajili wa majira ya kiangazi lililopita, wachezaji 40 walihusika kwenye usajili wa Chelsea, ambapo 12 walinaswa huko Stamford Bridge, wakati 28 walifunguliwa mlango wa kutokea, huku usajili wao ukifikisha Pauni 1 bilioni ndani ya mwaka mmoja tu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement