PESA YA COUTINHO IMEPELEKA MATAJI ANFIELD
Miaka 6 imepita sasa tangu klabu ya Liverpool ilipotangaza kumuuza mchezaji wao Philippe Coutinho kwenda kujiunga na klabu ya Barcelona kwa gharama ya £142 million.
Pesa ambayo klabu ya Liverpool iliipata baada ya mauzo ya Phillipe Coutinho ilitumika kununua wachezaji wawili Virgil van Dijk pamoja na Alisson Becker na baada ya hapo kla u hiyo ilifanikiwa kunyakua taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya "UEFA" pamoja na taji la ligi kuu ya England "EPL".