Manchester City wanaelekea katika pambano lao leo Jumamosi dhidi ya Crystal Palace wakiwa nyuma pointi tatu kutoka kileleni lakini kocha Pep Guardiola (53) amesema kikosi chake kinalenga kushinda mechi nane zilizobakia huku wakipiga dua wapinzani wao wateleze

City wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 67, pointi moja nyuma ya Arsenal wanaoshika nafasi ya pili na pointi tatu nyuma ya vinara Liverpool.

Ratiba iliyosalia ya ligi ya City ni pamoja na Luton Town iliyopanda daraja, Tottenham Hotspur, Brighton & Hove Albion, Nottingham Forest, Wolverhampton Wanderers, Fulham na West Ham United.

"Tusipofanya kazi yetu, haitatatua tatizo. Tunapaswa kushinda mechi nane zilizobaki. Ikitokea wapinzani wetu wakapoteza mechi, ni bora zaidi, lakini hatuwezi kuidhibiti.

"Kwa sasa tunapambania hatima yetu katika michezo yetu wenyewe" Alisema Pep





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement