Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa kwa sasa Manchester City imejidhatiti na haiwezi kuangusha pointi akitarajia Arsenal kushindwa mechi zao zilizosalia licha ya kudhihirisha uwezo wao.

Guardiola amesema wazi kuwa wanatamani Arsenal washindwe kwani hawawezi kudhibiti wanachofanya na kuweka wazi kuwa zimesalia mechi nne na hadhani kama wachezaji wake watakuwa wazembe kwa kupoteza pointi yoyote kwa sababu wanajua ni nini wanatakiwa kufanya.

Kuhusiana na Ligi kwa ujumla, Guardiola ameeleza kuwa Ligi imekuwa ngumu kuliko msimu uliopita nahii imetokana na ushindani kuongezeka kwa kila timu kuonyesha uwezo.

Kwa mchezo wa hapo jana dhidi ya Nottingham Forest, Pep Guardiola anatimiza jumla ya mechi mechi 300 alizoongoza za Premier League katika kipindi chake cha mafanikio makubwa kama Kocha.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement