Pazia la Ligi Kuu England linafungwa rasmi leo Mei 19, kwa michezo 10 huku macho na masikio ya wapenzi wa kandanda yakielekezwa kwenye michezo miwili ya kukata na shoka ambayo itaamua nani atakuwa bingwa wa Ligi hiyo kwa msimu huu wa 2023/24.

Mabingwa watetezi, Manchester City watakuwa nyumbani, Etihad kukabiliana na Wagonga nyundo West Ham United huku Washika Mitutu, Arsenal wakichuana na Everton kutafuta alama tatu ambazo zitaiwezesha kutwaa ubingwa ikiwa vinara, Man City watadondosha alama.

Manchester City wenye pointi 88 wanahitaji ushindi tu kutetea ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo bila kutegemea matokeo mengine. Kwa upande wao, Arsenal wenye pointi 86 wanahitaji ushindi huku wakiiombea dua mbaya Man City ili kutwaa ubingwa wa Ligi kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2003/2004.

Man City wakitoka sare huku Arsenal ikishinda basi ubingwa utaelekea Emirates kwa mara ya kwanza baada ya miongo miwili lakini historia inaibeba Man City kwa kuwa kwa misimu yote, timu ambayo ilingia uwanjani kwenye siku ya mwisho ya msimu ikiwa kileleni, basi ilinyakua ubingwa.

MECHI ZOTE ZA LIGI KUU UINGEREZA EPL ZITACHEZWA SAA 12:00 JIONI

Manchester City vs West Ham (Etihad)

Arsenal vs Everton (Emirates)

Brighton vs Manchester Utd (Amex)

Liverpool vs Wolverhampton (Anfield)

Chelsea vs Bournemouth (Stamford Bridge)

Brentford vs Newcastle (Brentford Community)

Burnley vs Nott’m Forest (Turf Moor)

Crystal Palace vs Aston Villa (Selhurst Park)

Luton vs Fulham (Kenilworth Road)

Sheffield Utd vs Tottenham (Bramall Lane)

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement