Klabu ya Paris Saint German imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Nchini Ufaransa (Ligue 1) baada ya klabu ya Monaco kupoteza 3-2 dhidi ya Olympique Lyon.

Monaco ambayo inakamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 haiwezi kufikia pointi 70 za vinara PSG hata kama itashinda mechi zake tatu zilizosalia kabla ya kufungwa kwa pazia la Ligi hiyo.

PSG imetwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa mara yao ya 12 kwenye historia ya Ligue 1.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement