Pambano la ndondi kati ya Mike Tyson na Jake Paul ambalo lilipangwa kufanyika Julai 20, 2024 limeahirishwa baada ya Tyson kupata changamoto za kiafya hali ambayo itaathiri ratiba yake ya mazoezi kwa wiki kadhaa zijazo. 

Pande zote mbili zimeafiki juu ya maamuzi hayo na inatarajiwa Tyson atarejea mazoezini wiki chache zijazo. 

Pambano hilo lisilo la ubingwa limetajwa kuwa ni sehemu ya burudani kwa kuwa Tyson ambaye atatimiza miaka 58 mnamo Juni 30, 2024 ameshastaafu, wakati mpinzani wake, Paul (27) ni staa wa michezo ya YouTube, Mwigizaji na aliingia kwenye ndondi Mwaka 2018. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement