PAMBA JIJI NA MIPANGO YA KURUDIDHA MAKALI WALIYO KUA NAYO MIAKA YA 1990-2002
KLABU Pamba Jiji kutokea jiji la mwanza imaanza mipango ya kuanza kuijenga timu shindani msimu ujao wa 2024/2025 kwajiri takuleta upinzani mkubwa.
PAMBA JIJI imepanga kulifimua benchi lake la ufundi na kutambulisha benchi jipya kwa maana walio pandisha timu hii baada ya miaka 23 hawana nafasi kwa msimu ujao.
Kocha Mbwana Makata pamoja na Renatus Shija inaelezwa hawatakua sehemu ya kikosi msimu ujao kwani wao wanahitaji kuleta kocha mpya ambae kimbinu atakua bora Zaidi,Mbali na kocha inaelezwa pia sehemu kubwa ya wachezaji wataondoka ikiwa kama sehemu ya maboresho.
Timu ambayo kwasasa ipo chini ya Harmashauri ya jiji la mwanza inamipango mikubwa yakurudisha UTAWALA kwenye mashindano makubwa Je,itafanikiwa kua bora maana tumeona pamba imekua ikijifunza kutoka kwa KLABU tofuati kama Simba SC,Yanga SC,Kmc, Dodoma jiji lengo la kujua namna ya kuendesha timu.