OSCAR PISTORIOUS AACHIWA HURU KUTOKA GEREZANI
Ulimwengu wa wapenda michezo baadaye leo utashuhudia tukio la kuachiwa huru kutoka gerezani mwanariadha wa zamani wa mbio fupi, Oscar Pistorious, Raia wa Afrika Kusini.
Pistorious anaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo kwa miaka isiyopungua tisa, na sasa ataenda kutumikia kifungo cha nje hadi mwaka 2029.
Oscar (37), alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi mara nne. Alimuua Reeva aliyekuwa ameingia ndani ya nyumba hiyo wakati Oscar akiwa bafuni.
Katika utetezi wake, nyota huyo alisema alifyatua risasi ikiwa ni sehemu ya kujihami kwani alidhani ni mwizi ameingia nyumbani kwake. Oscar amekuwa na maadui wengi tangu afanye tukio la mauaji na kupelekwa mahakamani, baadhi walijionyesha hadharani wakati kesi yake inasikilizwa kwenye mahakama ya North Gauteng High Court mwaka 2014.