ORLANDO PIRATES NA MAMELODI SUNDOWN ZATAWALA USIKU WA TUZO NCHINI AFRICA KUSINI
Baada ya msimu kutamatika Katika ligi ya south Africa yaani PSL, Nedbank, MTN 8 na Carlingknockout Hatimaye tuzo zimetolewa na tumeshuhudia klabu ya Orlando pirates ikitawala zaidi ikifuatiwa na Mamelodi sundown.
KATIKA tuzo hizo kulikua na vipengele vingi kweli kweli katika mashindano yote tajwa hapo juu, ambapo wachezaji wa Orlando pirates walitawala Zaidi PSL, MTN 8 na Nedbank.
Mfungaji bora alitoka Orlando pirates bwana Tshegofatso Mabasa 16 goals, mchezaji bora alitoka Mamelod sundown bwana Ronwell Williams akiwa ameshinda ligi kuu, AFL kipa bora,cosafa award kipa bora na afcon kipa bora, Kiungo bora akawa ni Patrick Maswanganyi kutoka Orlando pirates,kipa bora ni Ronwell Williams kutoka Mamelod sundown,Beki bora ni Grant Kekana kutoka Mamelod sundown na mchezaji bora chipukizi ni Relebohile Mofokengi
Tuzo nyingine kutoka MTN 8 mchezaji wa Orlando pirates ambae ndie kipa namba moja bwana Sipho Chaine alichukua tuzo hiyoo
Kwa upande wa Nedbank wachezaji wa Orlando pirates wametawala sana, mchezaji bora ni Patrick Maswanganyi na mchezaji chipukizi ni Relebohile Mofokengi
Kwa upande wa mashindano ya Carlingknockout mchezaji bora ni Devin Titus kutoka Stellenbosch
Kwa upande wa kocha tuzo imeenda kwa Rhulan Mokwena wa Mamelodi sundown
Upande wa refa ni bwana Sikhumbuzo Gasa na msaadizi wake bora ni Romario Phiri
Sasa hizo ni baadhi ya tuzo ambazo zilikuwa zinatolewa kwani kulikua na vipengele vingi sanaa lakini hivyo ni vile vipengele vya muhimu sana