Mchezaji Andreas Brehme, ambaye alifunga aliyefunga bao la ushindi kwa taifa la Ujerumani Magharibi katika Kombe la Dunia la mwaka 1990, amefariki akiwa na umri wa miaka 63.

Gazeti la kutoka ujerumani la Bild liliripoti kwamba Brehme alifariki siku ya Jumatatu usiku huko katika mji wa Munich, inaonekana kuwa alipatwa mshtuko wa moyo. 

Brehme aliripotiwa alipelekwa kwenye chumba cha dharura cha kliniki kwenye mtaa wa Ziemssenstrasse, karibu na nyumba yake, lakini hakuweza kupona.

Brehme, amefunga mabao manane, tulimshuhudia akicheza kwenye Kombe la Dunia la 1986, 1990 na 1994 na Mashindano ya Europa ya 1984, 1988 na 1992.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement